Sheikh
mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini, Bakari Mketo amefariki dunia ghafla
makaburini mara baada ya kuswalisha swala ya mazishi katika makaburi ya
Nonde jijini na mkoani Mbeya jioni ya jana.
Sheikh
huyo maarufu kwa jina la Mketo mkazi wa Nonde anayekadiriwa kuwa na
umri wa kati ya miaka 50-60 amekutwa na mauti katika eneo la makaburi
hayo ya Nonde mara tu baada ya kumaliza kutoa mawaidha kwa watu
waliojumuika kumzika mama aliyefariki katika hospitali ya rufaa Mbeya
juzi na msiba wake kuwekwa nyumbani kwake Sokomatola katikati ya jiji la
Mbeya.
Inaelezwa kuwa shekhe Mketo alitoa huduma zote tangu mwanzo wa msiba mpaka alipokutwa na mauti.
Kwa
mujibu wa mashuhuda ya kifo cha sheikh Mketo waliokuwa katika makaburi
hayo, wamesema kuwa marehemu Mketo hakuwa na dalili zozote za ugonjwa na
wala hakulalamika kujisikia vibaya kabla ya kukutwa na mauti hayo.
Aidha
mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa wakati akitoa mawaidha makaburini
hapo sheikh Mketo alisisitiza sana juu ya vijana kujifunza na kuifuata
vema elimu ya kiislamu na kuishika vilivyo kwani kifo hakina taarifa na
akatolea mfano kuwa hata yeye anaweza kukutwa na mauti papo hapo katika
eneo la makaburi na akalisisitiza hili zaidi ya mara tatu ndipo muda
mfupi baadaye akadondoka na kupoteza maisha yake.
Post a Comment