Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum
Hivi karibuni Sheikh Salum alikaririwa na gazeti mmoja (siyo
NIPASHE), akiwataka Waislamu nchini kumpuuza Mbunge huyo kwani ni
mfitinishaji kwa Waislamu.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Bunge, Haji
alisema licha ya Bakwata kuwa ni chombo cha kutetea maslahi ya Waislamu
na kuwaweka katika masuala ya kiroho lakini kutokana na uongozi mbovu
kwa sasa chombo hicho kimegeuka kuwa ni mtetezi wa viongozi wa kisiasa
na kuwakingia kifua viongozi wa serikali.
Alisema amelazimika kutoa kauli hiyo kufuatia Sheikh Salum kumwita
mbunge huyo mfitini kutokana na kutokubaliana na utendaji wa chombo
hicho ambacho kwa sasa kinaonyesha kukiuka maadili ya Bakwata na
kujiingiza katika siasa.
“Bungeni niliwahi kusema kuwa Bakwata ni taasisi ya kinafiki kwa
waislamu…kauli yangu hii itabaki kuwa pale pale na wala sitoibadilisha,”
alisema na kuongeza:
“Nasema kuwa viongozi wengi wa Bakwata kazi yao kubwa ni kusubiri
kupokea kondoo kutoka Uarabuni kwa ajili ya kuchinja huku wakijinufaisha
wao viongozi badala ya kuangalia ni jinsi gani ya kuwasaidia waumini wa
dini ya Kiislamu.”
Alisema waumini wa dini hiyo wanatakiwa kumpuuza Sheikh huyo kutokana na kauli zake ambazo anazitoa juu yake (Haji).
CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment