THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Taratibu
za Tiba za Rais zakamilika
Taratibu za matibabu ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, zimekamilika leo,
Jumatatu, Novemba 24, 2014.
Taratibu hizo za matibabu za Mheshimiwa Rais
Kikwete zimekamilika kiasi cha saa 12 asubuhi ya leo wakati madaktari bingwa
katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko mjini Baltimore, Jimbo la Maryland,
Marekani, walipomfanyia hatua ya mwisho ya tiba.
Hata hivyo, Rais Kikwete ataendelea kupumzika na
kuangaliwa kwenye Hoteli Maalum inayohusiana na Hospitali ya Johns Hopkins kwa
siku mbili hadi tatu kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani.
Kama kila kitu kitakwenda kama ilivyopangwa na
madaktari, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nyumbani Jumamosi, Novemba 29,
2014.
Rais Kikwete aliondoka nchini Alhamisi ya Novemba
6, 2014, kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya yake lakini madaktari katika
Hospitali ya Johns Hopkins waliamua kumfanyia upasuaji wa tezi dume Jumamosi ya
Novemba 8, 2014.
Rais Kikwete anaendelea kuwashukuru Watanzania kwa
sala na maombi yao ya kumtakia heri ya kupona haraka na kurejesha afya njema
katika kipindi chote cha ugonjwa wake.
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
24
Novemba,2014
Post a Comment