Uuzaji mchanganyiko wa tiketi
zaelektroniki kwenye Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) utakoma baada ya mechi
mbili za wikiendi hii kati ya Yanga na Mgambo Shooting na Simba na Ruvu
Shooting zitakazochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ligi itasimama kupisha mechi ya
Kalenda ya FIFA, mashindano ya Chalenji na dirisha dogo la usajili.
Baada ya hapo tiketi zote zitauzwa kwa njia ya mtandao, hivyo
hakutakuwepo na vibanda vya kuuza tiketi viwanjani.
Post a Comment