Mwanajeshi aliyemuua Osama bin Laden ametambulika kwa mara ya kwanza jana.

Anaitwa Rob O’Neill, 38, aliyewahi kufanya mission za kijeshi zaidi ya 400.
Baba yake, Tom O’Neill anasema: “Watu wanauliza kama tunaogopa kwamba
ISIS watakuja na kututeka kwasababu Rob anafahamika sasa. Nasema
nitachora target kubwa kwenye mlango wangu wa mbele na kusema ‘njooni
mtuteke’.
O’Neill mwenyewe alipongezwa na rais Barack Obama kwa kumuua bin
Laden kwa risasi tatu juu ya paji lake la uso wakati wanajeshi wa
Marekani waliposhambulia kambi yake huko Abbottabad, May 2, 2011.
O’Neill amekubali kufanyiwa mahojiano exclusive na kituo cha Fox baadaye mwezi huu.
Mission zake tatu alizozifanya zimetumika kwenye filamu za action za
Hollywood. Alikuwa mwanajeshi aliyeongoza wenzie huko kuokoa meli ya
Maersk Alabama, iliyokuwa imetekwa na maharamia wa Somalia ambapo
operesheni hiyo ilizaa filamu ya Captain Phillips.
Alisaidia pia kuokolewa kwa Marcus Luttrell, mtu aliyeishi kusimua
mpango uliofeli wa kumkamata kiongozi wa Taliban na kuzaliwa kwa filamu
‘Lone Survivor.’
Na pia alikuwa mtu aliyemuua Bin Laden kwenye Zero Dark Thirty.
Post a Comment