GARI lililokuwa
likisindikiza mzigo nyeti limepinduka leo likijaribu kumkwepa mwendesha
pikipiki na kuua waliokuwemo na kujeruhi wengine.
kamanda wa polisi mkoa wa
mwanza, Valentino Mlowola amethibitisha
kuwepo kwa ajali hiyo.
Amesema ajali hiyo
imetokea leo majira ya saa 7.40 katika eneo la Mkuyuni, jijini hapa ambapo
ilihusisha gari la Benki
Kuu (BOT) lenye usajili namba SU 35296 toyota land cruiser.
Alisema waliokufa ni Beatrice Wanzagi Lumereja (37) afisa wa BOT na
mkazi wa Kiseke na Dereva Mohamed Mumba (45).
Waliojeruhiwa na kulazwa
katika hospitali ya rufaa ya Bugando ni pamoja na Sajenti
Joel na PC Jumane
waliokuwa wakisindikiza mzigo huo nyeti pamoja na dereva pikipiki
Deus Kalokola (32).
Alisema chanzo cha ajali
hiyo ni dereva wa pikipiki namba T 792CTGkuingilia msafara
ghafla.
Hata hivyo Mlowola
alisema mzigo huo nyeti upo salama na kwamba miili ya marehemu
imehifadhiwa katika
hospitali ya Bugando.
Post a Comment