Wafanyabiashara wa UG waionya Kenya

Wafanyibiashara wa Uganda wameonya kuihama bandari ya Mombasa kutokana na ada mpya za mara kwa mara.
Wafanyibiashara wa Uganda chini ya muungano wa Wanabiashara wa mji wa Kampala Uganda KACITA wamelipa Shirika la ukusanyaji Ushuru nchini kenya KRA wiki mbili kuitoa mizingo yote inayoelekea Uganda la sivyo waigomee bandari ya Mombasa.
Ilani hiyo iliafikiwa siku ya Alhamisi baada ya saa kadhaa za majadiliano kuhusu athari za hatua ya KRA ya kutoza kodi bidhaa zote zinazoingia katika badari hiyo.
Awali ,wafanyibiashara walikuwa wakilipa ada wanayotozwa wakati wanapochukua mizigo yao pamoja na ada nyenginezo.
Hatua hiyo kulingana na KACITA si kinyume na matarajio ya jumuiya ya Afrika mashariki pekee bali pia inawaumiza wafanyibiashara wa Uganda pamoja na uchumi.
Mwenyekiti wa KACITA Everest kayondo amesema kuwa kufikia jumatano kulikuwa na makasha 4,000 yanayozuiliwa katika Bandari ya Mombasa kutokana na ada za mara kwa mara zinazotolewa na KRA.
''Kwa hivyo tunaipa KRA wiki mbili kutoa mizigo yote ya Uganda la sivyo tuhame hadi katika bandari ya Dar es Salaam'',.aliongezea
Wafanyibiashara hao pia walikubaliana kwamba iwapo mahitaji yao hayataafikiwa ,wataishinikiza serikali ya Uganda kuzuia bidhaa za kenya zinazoingia katika soko la Uganda.
- BBC

Post a Comment

Previous Post Next Post