
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Stephen Kebwe.
Na Beatrice Lyimo- Maelezo
Serikali
imetoa wito kwa kila mwananchi nchini kuhakikisha kwamba anapima afya
yake mara kwa mara kwa kuwa ugonjwa wa kisukari unaweza usionyeshe
dalili yoyote mapema ili kuweza kukabiliana na kupunguza athari za
ugonjwa huo
Aidha
Serikali imesisitiza kuwa endapo mtu atatambulika kuwa ana ugonjwa
huo, atumie huduma za afya kulingana na ushauri wa atakaopewa na
wataalam wa afya.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.
Stephen Kebwe leo alipokuwa anatoa tamko kuhusu Siku ya Kisukari Duniani
itakayoadhimishwa Novemba 14, mwaka huu duniani kote yenye kauli mbiu
“Ulaji unaofaa, huanza na mlo wa asubuhi”.
Siku
ya kisukari duniani ilianzishwa baada ya kuona ugonjwa wa kisukari
unaongezeka sana duniani kote na Tanzania kama nchi nyingine duniani
huadhimisha siku hii kwa kushirikiana na Chama cha Ugonjwa wa Kisukari
Tanzania kutoa elimu ya umuhimu wa kuzuia na kujikinga na madhara
mbalimbali yatokanayo na ugonjwa huu, alisema Naimu Waziri.
“Ugonjwa
wa Kisukari ni hali ambayo hutokea wakati sukari katika damu inapokuwa
nyingi kupita kiwango cha kawaida kwa muda mrefu” aliongeza Dkt Kebwe.
Amebainisha
kuwa asilimia 80 ya wagonjwa wa kisukari ulimwenguni wanaishi katika
nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania, na tafiti zinaonyseha kuwa mwaka
2007 kulikuwa na wagonjwa 246 milioni duniani,mwaka 2012 wagonjwa
milioni 371, mwaka 2013 wagonjwa milioni 382ulimwenguni kote na mwaka
2013 kulikuwa na wagonjwa milioni 19.8 barani Afrika.
Aidha
nchini Tanzania kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2012 na
kuhusisha wilaya 50 ulionyesha kuwa asilimia 9.1 ya Watanzania wenye
umri wa miaka 25 na kuendelea wana ugonjwa wa kisukari.
Dk.
Kebwe aliongeza kuwa takwimu za watoto wenye kisukari mwaka huu ni
kati ya asilimia 15 mpaka 20 ya wagonjwa wa kisukari ambao wanatibiwa
kwenye kliniki za hapa nchini.
“Lakini
wapo wengine hawajitokezi kwenye kliniki kwa sababu mbalimbali zikiwemo
imani potofu, gharama pamoja na umbali wa huduma za afya zilizopo”
aliongeza Naibu Waziri huyo.
Aidha
Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaendelea na
utekelezaji wa Sera ya Afya(2007) inayolenga kutoa huduma kwa magonjwa
yasiyoambukiza ikiwemo kisukari kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa
ndani ya Nchi na wa kimataifa.
Tanzania
inaungana na mataifa yote duniani kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa
la mwaka 2011 la kuhakikisha magonjwa yasio ya kuambukiza yanapungua
kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2025.
Post a Comment