Wassira
alisema mwaka 2010 CCM ilifanya makosa katika baadhi ya maeneo kwa
kusimamisha wagombea wasiokubalika, hatua ambayo ilisababisha chama
kupoteza majimbo na kata ambazo zilichukuliwa na upinzani.
“Naomba
makosa ya mwaka 2010 yasijitokeze tena kwa kuwachagua watu wasiopendwa
na wananchi, hali hiyo inaweza kusababisha nafasi za wenyeviti wa
setikali za mitaa na vitongoji zikaenda kwa wapinzani,’’ alisema.
Wassira
alitoa tahadhari hiyo alipokuwa akifungua mkutano uliowashirikisha
majumbe kutoka Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Pwani.
Alisema
mwaka 2010 makosa yalijitokeza kwa kupitisha majina ambayo wananchi
hawakutaka yarudi na kusema kuwa kosa hilo lisirudiwe mwaka huu bali
wapitishe majina yanayokubalika. “Kama hamtayafanyia kazi majina hayo, mjue wapinzani watazichukua nafasi hizo,” alitahadharisha.
“Tusiangalie
mtu aliyeshinda kwa kupata alama nyingi, kinachotakiwa ni kuangalia
huyo anakubalika kwa jamii na anavigezo vyoye kama hakubaliki inabidi
asichukuliwe, mkifanya maamuzi yasiyo sahihi, mtasababisha chama kukosa
ushindi,’’ aliongeza.

Post a Comment