Watu
watatu wamenusurika kuuawa na wananchi wa kijiji cha Ndoombo kilichoko
kata ya Nguarisambo wilayani Arumeru mkoani Arusha baada ya kukutwa
wakiwa wamekata miti na kupasua mbao katika chanzo cha maji cha wananchi
hao .
Katika sakata hilo watuhumiwa hao ambao pia wamekamatwa na vipande
150 vya mbao wamesema wao walipewa kazi ya kuhamisha mbao hizo na
kwamba wenye mali wamekimbia.
Baadhi ya wananchi waliosaidia kubainika kwa uharibifu huo wamesema
walishtushwa na mlio wa mashine za kupasulia mbao ndani ya msitu huo na
walipofuatilia ndipo wakakuta tayari watu hao wameshakata idadi kubwa
ya miti na kupasua mbaohizo.
Viongozi wa vijiji kata na wilaya hiyo wamesema wamekubaliana
kuzigawa mbao zilizokamatwa kwa vijana waliofanikisha zoezi hilo hatua
inayolenga kuongeza chachu ya kulinda vyanzo vya maji na wamewataka
vijana kote nchini kutowafumbia macho watu wanaoharibui vyanzo vya maji
na wezi wa rasilimali zingine za asili.
- ITV
Post a Comment