Wizara yakwamisha ufadhili Shule ya Miono

Picha Na:- Maktaba
Bagamoyo. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inadaiwa kukwamisha ufadhili wa Sh200 milioni katika Shule ya Sekondari ya Miono Bagamoyo, kwa mchepuo ya Sayansi, baada ya kompyuta zaidi ya 10 zilizotolewa na Kampuni ya Wakefield and Cushman ya Ubelgiji kupotea wizarani katika mazingira tata.
Licha ya kupotea kwa kompyuta hizo hadi sasa hakuna maelezo yoyote kutoka kwa viongozi wa Mkoa wa Pwani.
Taarifa za upotevu wa komputa hizo imebainika jana wakati wa ziara ya wafanyabishara kutoka Ubelgiji katika maeneo ya uwekezaji (EPZ) kuona hali ya miundombinu iliyopo.
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Dk Deodorus Kamala alisema amesikitishwa na baadhi ya watendaji na viongozi wanaotekeleza majukumu yao kinyume na taratibu na kanuni za utumishi wa umma.
Alisema Kampuni ya Wakefield and Cushman, ilifanya kazi nzuri kwa kushirikiana na Serikali kusaidia wananchi wa Pwani kujenga shule hiyo hadi kukamilika.
Balozi Kamala alisema kutokana na kompyuta hizo kupotea, kampuni hiyo imesitisha misaada shuleni hapo kwa muda.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza alisema ameshtushwa na taarifa hiyo na kuahidi kuwasiliana na Wizara ya Elimu ili ajue kwa nini mzigo huo haujafika kwenye shule hiyo.
“Balozi nimesikitishwa sana na kitu hicho siku ya leo (jana), ila nakushukuru kutuletea ujumbe wa wahisani wetu,” alisema.

Post a Comment

Previous Post Next Post