Mkurugenzi
wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa jijini Dar
es salaam, Bw. Moses Malaki (kulia), akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani), wakati wa hafla ya kukabidhiwa mabango
yanayotahadharisha wananchi na wageni waingiao na watokao Tanzania
kutojihusisha na shughuli yoyote inayohusiana na ujangili wa wanyama
(kushoto), Mkurugenzi wa WWF Tanzania Bw. Bell’Aube Houinato.(PICHA NA
PHILEMON SOLOMON).
Shirika
lisilokuwa la kiserikali linalojihusisha na uhifadhi wa mazingira na
wanyama pori la World Wide Fund for Nature (WWF), limejiunga katika
jitihada za kitaifa na kimaifa za kupambana na ujangili nchini ambapo
pamoja na mambo mengine limetoa mabango yanayotahadharisha wananchi na
wageni waingiao na watokao Tanzania kutojihusisha na shughuli yoyote
inayohusiana na ujangili wa wanyama.
Akikabidhi
vifaa hivyo Novemba 27, 2014 jijini Dar es Salaam kwa Mkurugenzi wa
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa jijini Dar es
salaam ,Bw.Moses Malaki,Mkurugenzi wa WWF Tanzania Bw. Bell’Aube
Houinato, aliwataka jamii za ndani na za kimataifa kuhakikisha
zinaongeza jitihada ili kuhifadhi rasilimali hizo kwa manufaa ya sasa na
kizazi kijacho.
Mkurugenzi
wa WWF Tanzania Bw. Bell’Aube Houinato akisisitiza jambo kuhusiana na
vyombo vinavyohusika na ulinzi na uangalizi wa rasilimali za nchi.
”
Jukumu la kumaliza kadhia hii ya biashara haramu ya nyara za umma ni la
wote si la serikali pekee au WWF bali umma mzima wa Tanzania na
kimataifa,hivyo kila mmoja kwa sehemu yake na eneo lake awajibike
ipasavyo”,alisema Bw.Houinato.
Aidha,aliongeza
kuwa ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha vyombo vinavyohusika na
ulinzi na uangalizi wa rasilimali zetu vinajengewa uwezo wa kimaarifa na
kivifaa ili kuhakikisha vyombo vyote vinatimiza wajibu wake kwa tija
kubwa.
Kwa
miaka ya hivi karibuni nchini Tanzania,kumeibuka tatizo la ujangili
ambapo mauaji a Tembo na Faru yameongezeka huku jitihada za kimataifa na
kitaifa zikiwa zinaonekana kulegelega jambo lililozishtua jamii za
kimataifa hivyo kujiunga na kuongeza bidii katika vita hiyo.
Mkurugenzi
wa WWF Tanzania Bw. Bell’Aube Houinato (kulia), akimkabidhi Mkurugenzi
wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa jijini Dar
es salaam, Bw.Moses Malaki moja ya mabango hayo.
Waandishi
wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere wa jijini Dar es salaam, Bw.Moses Malaki (meza
kuu kulia), wakati wa hafla hiyo.
Muonekano
wa moja ya mabango hayo yenye luga tatu ambayo yatawekwa sehemu
mbalimbali ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa
jijini Dar es salaam.
Post a Comment