Marehemu Shem Ibrahim Kalenga enzi za uhai wake.
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za
msiba wa msanii nguli wa tasnia ya muziki wa Dansi nchini Shem Ibrahim
Kalenga
“
Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo hiki
cha Shem Ibrahim Kalenga ambaye mchango wake katika muziki wa Dansi ni
mkubwa mno na unahitajika sana, pengo aliloliacha ni kubwa kwani
ubunifu wake bado unahitajika katika tasnia hii.” Baraza linatoa pole
kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha tunawatakia moyo
wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.
Mwenyezi
Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko
pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Imetolewa na
Godfrey Mngereza
Kaimu Katibu Mtendaji
Baraza la Sanaa la taifa.
Post a Comment