Mjumbe
wa kamati ya utendaji CHADEMA manispaa ya Singida, Vicent Mughwai
(katikati) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kusudio la
chama hicho kumfungulia shitaka msimamizi wa uchaguzi wa serikali za
mitaa manispaa ya Singida, kwa tuhuma ya kukiuka kanuni za uchaguzi huo.
Vicent ndugu yake na mbunge wa jimbo la Singida mashariki na mnadhimu
mkuu wa sheria CHADEMA, Tundu Lissu, ametangaza rasmi kumng’oa mbunge wa
CCM jimbo la Singida mjini Mohammed Gullam Dewji, kwenye uchaguzi mkuu
ujao. Kulia mjumbe wa kamati ya wilaya na katibu kata CHADEMA kata ya
Unyambwa na kushoto ni mwenyekiti wa baraza la wazee wilaya CHADEMA
Singida mjini.
Na Nathanlei Limu, Singida
CHAMA
Cha Maendeleo na Demokrasia (CHEDEMA) halmashauri ya manispaa ya
Singida, kinatarajia kumburuza mahakamani msimamizi wa uchaguzi wa
serikali kutokana na tuhuma mbalimbali, ikiwemo ya uchakachuaji wa kura.
Hayo
yamesemwa na mjumbe wa kamati ya utendaji CHEDEMA manispaa ya
Singida,Vicent Mughwai,wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari
iliyohusu uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika Desemba 14 mwaka
huu.
Alisema
zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa manispaa ya Singida, kwa kiasi
kikubwa haukufanyika kwa haki. Vitendo vya rushwa na ukiukwaji kuanzia
uandikishwaji wa wapiga kura na ukiukwaji mkubwa wa kanuni za uchaguzi
na wa kupata wagombea nafasi za uongozi na mchakato wa kupata viongozi
na chaguzi mkuu.
Vicent
alitaja baadhi ya vitendo vya ukiukwaji wa kanuni kuwa ni wasimamizi wa
CHADEMA kuenguliwa kwenye nafasi ambazo walitaka kuja kuwatumikia
wananchi kikamilifu, kwa lengo la wagombea wa CCM waweze kupita bila
vikwazo vyovyote.

Baadhi
ya viongozi wa ngazi mbalimbali CHADEMA manispaa ya Singida, wakiwa
kwenye mkutano wa chama hicho na waandishi wa habari ambapo CHADEMA
walitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya uchaguzi wa serikali za
mitaa,vijiji na vitongozi uliomalizika Desemba 14 mwaka huu.
Mjumbe
huyo alitaja vitendo vingine kuwa kada wa CCM kutumia gari kusomba watu
na kuwapeleka kwenye vituo vya kupigia kura na wagombea wa CHADEMA
kuzuiwa kuingia kwenye vyumba vya kuhesabia kura ili uchakachuaji uweze
kufanyika kitendo ambacho ni kinyume na kanuni namba 22.
“Kutokana
na ukiukwaji mkubwa wa kanuni za uchaguzi katika jimbo letu,tunaomba
vyombo husika na serikali,vifanye uchunguzi wa kina na hatua kali
zichukuliwe dhidi ya wote watakaobainika wana hatia”alisema.
Aidha,
mjumbe huyo alisema CHADEMA inamwomba Waziri wa TAMISEMI, amchukulie
hatua kali msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa ambaye ni
mkurugenzi wa manispaa ya Singida,kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake
kusimamia ipasavyo uchaguzi huo.
“Tunawasiliana
na wanasheria wa chama chetu ili tuweze kuchukua hatua za kisheria
kupinga matokeo yote yaliyopatikana kutokana na ukiukwaji mkubwa wa
kanuni.Lengo ni wapiga kura wetu waweze kutendewa haki”,alifafanua.

Baadhi
ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliohudhuria kikao
kilichoitishwa na CHADEMA manispaa ya Singida kutangaza nia ya
kumfikisha mahakamani msimamizi wa uchaguzi huo manispaa ya Singida,
kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo ya vitendo vya rushwa kwa ajili
ya kukidhoofisha CHADEMA.(Picha na Nathaniel Limu).
Kwa
upande wa msimamizi wa uchaguzi serikali za mitaa manispaa ya Singida,
Joseph Mchina, alisema CHADEMA wanao haki ya kwenda mahakamani, ili
waweze kupatiwa haki yao kama wanaamini kulikuwepo na ukiukwaji wa
kanuni na vitendo vya rushwa katika uchaguzi huo.
“Mahali
ambapo wagombea wa CHADEMA hawakuruhusiwa kuingia kwenye vyumba vya
kuhesabia kura, nafasi ilikuwa finyu lakini mawakala wao
waliruhusiwa.Viongozi wa CHADEMA ambao walikuwa sio wagombea wala
wasimamizi, kanuni hazitoi nafasi kwao kuingia kwenye vyumba vya
kuhesabia kura,l akini wao walilazimisha waingie kitendo ambacho
hakikubaliki”,alisema Mchina.

Post a Comment