Marekani
na Cuba zimetangaza kukomesha uhasama wa miaka hamsini na kufungua
mwanya wa mazungumzo ya kidiplomasia ili kurejesha uhusiano kati yao.
Akitoa
tangazo hilo la kihistoria Rais Barrack Obama, amesema kuwa mfumo wa
Marekani wa kuitenga Cuba, umeshindwa. Mjini Havana, wanafunzi walitoka
madarasani na kuanza kuimba huku wakipeperusha vijibendera hewani na
kupiga kengele kila mahali majiani, ishara ya kupokea vyema tangazo hilo
la Obama..Rais wa Cuba Raúl Castro, ameiomba Marekani kuvunjilia mbali vikwazo vya miaka mitano vya kiuchumi dhidi ya Nchi yake, ambayo anasema vimeiletea nchi hiyo madhara makubwa. Kuondolewa kwa vikwazo hivyo vitahitaji kupitishwa na Bunge la Congress la Marekani, ambalo linaongozwa na wanachama wengi wa chama pinzani cha Republican. Wengi wao wanapinga ulegezaji kamba kwa vikwazo.(BBC)
Post a Comment