TABIA
za mitoko ya usiku matembezini, uvaaji viatu virefu na unywaji pombe
unaofanywa na wamama wajawazito, kama alivyo sasa muigizaji Aunt
Ezekiel, zimeelezewa kuwa si nzuri na zina uwezekano mkubwa wa
kusababisha madhara kwa mtoto anayetarajiwa kuzaliwa.
Mkali katika tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel.
Akizungumza
baada ya kuulizwa na gazeti hili juu ya mwenendo wa muigizaji Aunt
Ezekiel ambaye mara kadhaa huonekana akiwa ‘viwanja’ usiku, daktari
mtaalamu wa magonjwa ya kina mama na watoto, aliyejitambulisha kwa jina
moja la Dokta Chale, alisema utokaji wa usiku na uvaaji wa viatu virefu
unaweza kusababisha matatizo ya nyonga, shida wakati wa kujifungua,
miguu kuuma na uvimbe kwenye vifundo vya miguu ‘enka’.
Kuhusu
unywaji pombe, Dokta Chale alisema endapo mama mjamzito atafanya tabia
hiyo, ipo hatari ya uelewa wa mtoto katika ukuaji wake kuwa mdogo na pia
kuchukua tabia zote za mama yake.
...Akizidi kujiachia.
“Viatu
virefu na mitoko ya usiku kwa mama mjamzito ina madhara makubwa sana
kwani mtoto atakuwa na uelewa mdogo, yaani akili yake inakuwa haikui
sawasawa, kifupi ana-adapti (kuiga) tabia zote za mama yake anaweza kuwa
zezeta kama mama anatumia pombe,” alisema.
Katika
kudhihirisha kuwa ustaa ni kazi kubwa, licha ya ujauzito wake kuonekana
mkubwa, Aunt Ezekiel amekuwa akijirusha kama kawaida sehemu mbalimbali
nyakati za usiku huku wakati mwingine akiwa amevaa viatu virefu.
Post a Comment