Basi
liitwalo Easy Bus lenye namba za usajili T 298 BLZ lililokuwa
likitokea Lilongwe Malawi likiwa katika mtaro wa Mlima Kitonga.
Jitihada zikifanyika kulivuta basi hilo.
Foleni kubwa iliyosababishwa na basi hilo baada ya kuingia mtaroni na kuziba njia.
Basi la abiria lenye namba za usajili T 298 BLZ likiwa linatolewa katika mtaro wa Mlima Kitonga mapema leo baada ya kutumbukia.
Hali hii imesababisha foleni kubwa kwa magari huku mengine
yakishindwa kuendelea na safari zake. Kwa mujibu wa mashuhuda, chanzo
cha gari hilo kutumbukia mtaroni ni kufuatia kupata hitilafu na hatimaye
uamuzi wa kuliegesha kando ukafanyika kisha abiria wote wakashuka ili
kusubiri marekebisho hayo.
Haikupita muda mrefu baada ya abiria kushuka gari lilikosa balansi,
likaanza kurudi kinyumenyume na kisha kuingia mtaroni. Hakuna mtu
aliyefariki dunia wala kujeruhiwa katika ajali hiyo.
Post a Comment