GORAN AMWAGA WINO KWA MWAKA MMOJA KUINOA SIMBA

KOCHA mpya wa Simba raia wa Serbua Goran Kopunovic amemwaga wino wa mwaka mmoja kuinoa timu hiyo ya Msimbazi.

Mmoja wa viongozi wa Simba aliiambia blog ya jamii kuwa kocha huyo aliyewasili leo asubuhi na kufikia kwenye hotel ya Double Tree Masaki ataondoka kesho kwenda Zanzibar kujiunga na timu hiyo ya wekundu wa Msimbazi inayoshiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Naye Kopunovic akizungumza muda mfupi baada ya kukanyaga hardhi ya Tanzania alisema "Nimekuja kufanya kazi, naamini nitapata ushirikiano kutoka kwa viongozi wa Simba, wachezaji na mashabiki, Simba ni timu kubwa, naamini nitawapa mafanikio."alisema

Kocha huyo, amechukua mikoba ya Patrick Phiri aliyefungashiwa virago baada ya uongozi wa Simba chini ya mwenyekiti wake Evans Aveva kufanya tathmini ya mwenendo wa timu ambapo ametoka sare mechi sita, ameshinda mechi moja na kupoteza moja hivyo kuona hastaili kuendelea kuinoa timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi huku akidaiwa kukaidi agizo la viongozi la kutowachezesha Waganda katika mechi dhidi ya Kagera walionyukwa bao 1-0

Post a Comment

Previous Post Next Post