Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Gedion M Kimilu.
JESHI la Polisi nchini Kenya leo limetoa majina ya watuhumiwa wawili wanaosakwa kwa kuhusika katika shambulio la kigaidi la Mandera ambao ni Mohamed Mohamud aka Dulyadin aka Gamadheere kutoka Garissa na Ahmed Iman kutoka Majengo jijini Nairobi.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi nchini Kenya leo.
Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Gedion M Kimilu imewaelezea watu hao kuwa mihimili ya Kundi la Kigaidi la Al Shabaab na wanasakwa kwa udi na uvumba kwa kuhusika katika matukio kadhaa ya kigaidi nchini humo.
DCI Kimilu amesema; "Mtu yeyote mwenye taarifa za watu hawa awasiliane na kituo cha polisi kilicho karibu naye ili wakamatwe maana ni watu hatari"
Post a Comment