Hili ni jiji la Sundsvall nchini Sweden.
Mji huu unaoendeshwa na manispaa ya Sundsvall umeanzisha mahusiano na
wadi za Makunduchi yenye lengo la kuiweka Makunduchi kwenye ramani ya
dunia kwa upande wa elimu. Mji huu umeanzishwa mwaka 1621 na mfalme
Gustav ll Adolf ambaye alikuwa kiongozi shupavu kijeshi.
Lengo la mtawala huyu ni kuigeuza Sweden
kuwa dola yenye nguvu duniani. Kiuchumi mji huu ulitegemea kuuza mbao.
Hata nyumba zake za enzi hiyo zilikuwa za mbao. Mwaka 1888 mji huu
uliteketezwa kwa moto na kubakia jivu tupu.
Hali hii ilipelekea kuachana na ujenzi
wa nyumba za mbao katikati ya jiji na hapo ndipo jina la mji wa mawe
(stone city) likajitokeza. Mabigwa wa ujenzi kutoka nchi mbali mbali za
Ulaya waliingia Sundsvall kujenga nyumba za Mawe ambazo hadi leo
zinaonekana mjini hapa.
Post a Comment