PAMOJA
na tetesi kuwa nguli wa filamu za Kibongo Blandina Chagula ‘Johari’,
ameshindwa kushika mimba, mwenyewe ameamua kufunguka na kudai kuwa
kizazi chake kinafanya kazi na anachosubiri ni kumpata mwanaume ambaye
atakuwa tayari kumuoa ndipo atakaporuhusu kuzalishwa.
Nguli wa filamu za Kibongo Blandina Chagula ‘Johari’.
Akizungumza
na Amani, Johari alisema kuwa endapo akitokea tayari yupo ndani ya ndoa
anaweza kufanya hivyo lakini kwa maneno ya watu kamwe watasubiri kwani
anaamini kizazi chake kipo imara na wakati wowote akiamua kushika mimba
kitafanya kazi.
“Kizazi
changu kinafanya kazi na mipango hiyo ya kushika mimba mimi siwezi
kukubali nipate mtoto kabla ya kuolewa, suala la kufanya jambo kwa lengo
la kuwafurahisha watu mimi siwezi kufanya hivyo,” alisema Johari.
Post a Comment