Jokate asaini mkataba wa thamani ya Sh8.5 bilioni na kampuni ya Kichina

Jokate na Guoxun wakionyesha mikataba baada ya kusaini


Mbunifu mavazi, Miss Tanzania wa namba mbili 2006,  mwanamuziki na muigizaji wa filamu, Jokate
Mwegelo amesaini makubaliano yenye thamani ya Sh8.5 billion na kampuni ya Kichina,  Rainbow Shell Craft Company Limited kwa ajili ya kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali za lebo yake ya Kidoti.Makubaliano hayo yalisainiwa leo kwenye hotel ya  Serena baina ya Jokate na Afisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya Rainbow Shell Craft Company Limited  (CEO), Deng Guoxun.


Akizungumza katika hafla hiyo,  Jokate alisema kuwa makubaliano hayo ni ya kudumu na kampuni hizo mbili zitazalisha na kuuza bidhaa za kidoti Tanzania nzima na nje ya mipaka yake.

Alifafanua kuwa kampuni ya China itawekeza Tanzania na kuwafaidisha watanzania kwa kutoa
nafasi ya ajira. Alisema kuwa pia wanatarajia kujenga kiwanda ili kuinua uchumi wa nchi na maisha ya watanzania.


 Jokate akiteta jambo na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa kwenye hafla hiyo


 “Hii ni hatua kubwa ya maendeleo kwangu, kama unavyojua, wakati naanza kujishugulisha na masuala ya urembo, ubunifu na uanamitindo, sikutegemea kufikia hatua hii ya kuingiza bidhaa zangu kimataifa,
lakini sasa, ndoto zangu zimetimia na najivunia mafanikio haya,” alisema Jokate.


Alisema kuwa mbali ya kutoa mitindo tofauti ya kisasa ya nguo, kampuni yake pia itazalisha
aina mbali mbali za viatu, nywele ikiwa pamoja na  mawigi,  weaving, Rasta na viatu vya wazi (sandals)
ambazo kwa sasa zipo tayari kwenye soko la Tanzania.



“Mpango wangu ni kupanua soko la bidhaa zangu kama Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Afrika
Kusini na nchi nyingine za Afrika,” alisema.


Afisa Mtendaji wa Guoxun alisema kuwa wamefurahi kukamilisha ubia na kampuni ya
Kidoti na haya ni matunda ya ushirikiano wa kudumu baina ya serikali yao naTanzania.

 

  “Tumefurahi sana kukamilisha makubaliano haya, tunatarajia kuongoza katika soko la hapa nchini na wenzetu (wachina) watafaidika pia, ” alisema Guoxun.
Source:Michuzi

Post a Comment

Previous Post Next Post