Maazimio ya Bunge yalimtaka Rais kuwawajibisha wote waliotajwa
kuhusika na kashfa ya escrow, uamuzi ambao upo mikononi mwa Rais Kikwete
Hatimaye Novemba 29, 2014 Bunge letu lilimaliza kikao muhimu sana pengine kuliko vikao vyote tangu lianze mwaka 2010.
Katika makala haya, ninafanya tathimini ya yale
yaliyojiri katika vikao vya 16 na 17 vya Bunge letu kwa kuzingatia
mafunzo yaliyojitokeza katika Bunge hili katika maeneo matatu, ambayo ni
mamlaka ya Bunge, kukua kwa demokrasia na nafasi ya kizazi kipya cha
wanasiasa.
Mamlaka ya Bunge.
Baada ya wabunge kutoa maoni yao katika Taarifa
iliyowasilishwa na Kamati ya Hesabu ya Serikali (PAC) na majibu ya
Serikali kama yalivyowasilishwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo, ilikuwa ni wazi kwamba Serikali ilikuwa imelemewa na
hoja za PAC.
Kulemewa kwa hoja za Serikali kulikuja kuwa wazi
zaidi baada ya Kamati ya PAC kujibu kwa umakini mkubwa hoja za Serikali
na wabunge waliokuwa wanaegemea upande wa Serikali.
Baada ya mjadala kuhitimishwa mambo matatu
yalikuwa dhahiri kwa wabunge wengi. Mosi, sehemu ya fedha zilizokuwa
katika akaunti ya Tegeta Escrow ilikuwa ni ya umma.
Pili, kuna baadhi ya viongozi wa Serikali na watu
wengine wenye mamlaka katika jamii walikuwa wamejipatia fedha ya Escrow
katika mazingira yanayotia shaka kuhusu maadili yao kama viongozi.
Tatu, Serikali haikutekeleza wajibu wake
kikamilifu katika kusimamia masilahi ya umma katika uendeshaji wa
akaunti ya Tegeta Escrow na mikataba ya nishati kwa jumla.
Kutokana na makosa haya ilikuwa lazima kwa Bunge
kuchukua hatua kadhaa katika kuiwajibisha Serikali na hapa ndipo hoja ya
mamlaka ya Bunge inapokuja.
Kutokana na mjadala wa Bunge usiku wa Ijumaa 28
Novemba 2014 ilikuwa wazi kwamba Bunge letu limewekewa mipaka mikubwa
sana kikatiba katika kuiwajibisha Serikali.
Pamoja na kwamba wabunge wengi walitamani kwa
usahihi kabisa kuwajibisha mara moja waliohusika na kadhia hii, lakini
walikuwa hawana uwezo wa kikatiba wa kutekeleza matamanio yao
- Mwananchi
Post a Comment