Stori: Waandishi Wetu HUKU
maajabu mengi yakiendelea kutokea kila kukicha na hivyo kuashiria
mwisho wa dunia unakaribia, mastaa kibao wa filamu wameonekana
kujisalimisha kanisani na kuhudhuria ibada ya kiroho ya Inuka Uangaze
maeneo ya Vatican -Sinza jijini Dar es Salaam.
Mc Pilipili.
Chanzo makini kilicho ndani ya kanisa hilo kilisema kwamba wasanii
wengi wamevutiwa na huduma hiyo ambayo maombi yake hufanyika kila
Jumanne na Jumatano na huongozwa na mchungaji mkuu, Buldoza Mwamposa.
Hosti wa kipindi cha 'Wanawake Live' cha chaneli Five, Joyce Kiria
Baadhi ya wanaotajwa kuonekana kanisani hapo ni pamoja na Dotnata,
Thea, Mainda, Mc Pilipili, Joyce Kiria na Dokii. Msemaji wa mchungaji
Mwamposa aliyejitambulisha kwa jina la Leonard Mwazembe alikiri nyota
hao kupata maombi kanisani kwake.
Post a Comment