MIMI SI MFUGA KUCHA KAMA WAO SABBY ANGLE

Stori: Hamida Hassan
STAA wa filamu za Kibongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angle’ amesema yeye si mfuga kucha kama mastaa wengine ambao hakuwaweka wazi majina yao na kudai kuwa yeye ni mwanamke anayejitambua.
“Mwenzao mimi napika kila aina ya chakula, linapokuja suala la nyumbani nafanya kila kitu si mwanamke wa kufanyiwa na wasichana wa kazi na kutuma kila wakati,” alisema Sabby.

Staa wa filamu za Kibongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angle’.
Sabby alisema mambo ya kufuga kucha na kutaka kuoshwa miguu kila wakati yeye anaona hayafai kwake pamoja na kuwa staa bado ataendelea kuwa na maisha yake ya kawaida tu kama mwanamke.

Post a Comment

Previous Post Next Post