.jpg)
Mtayarishaji wa tamthilia ya Siri ya Mtungi Louise Kamin kutoka Shirika Lisilo la Kiserikali la Media
for Development International Tanzania (MFDI-TZ) akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na msimu wa pili na wa mwisho
wa tamthilia hiyo. Kutoka kulia kwa Kamin ni Karabani (Muongozaji),
Cheche (Muigizaji), Jordan Riber (Muongozaji). Kutoka kushoto ni
Goldliver Gordian (cheusi) na David Michael (Duma).
.jpg)
Cheche akizungumza katika mkutano huo.
.jpg)
Muongozaji wa tamthilia hiyo, Karabani akisisitiza jambo katika mkutano huo.
.jpg)
Muongozaji , Jordan Riber akifafanua jambo katika mkutano huo.
Msimu
wa pili wa tamthilia ya Siri ya Mtungi itazinduliwa rasmi Desemba 7
kupitia televisheni ya Taifa (TBC). Akizungumza jijini leo mtayarishaji
wa tamthilia hiyo, Louise Kamin kutoka Shirika Lisilo la Kiserikali la
Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) alisema kuwa
sehemu ya pili ya tamthilia hii inakamilisha Siri ya Mtungi kufuatia
msisimko mkubwa wa msimu wa kwanza.
Kamin
alisema kuwa kukamilika kwa hatua ya pili kunatokana na udhamini mnono
wa the John Hopkins University Centre for Communication Programs (JHU
CCP) ambao walitoa uongozi wa elimu na mkakati katika tamthilia, taasisi
ya Misaada ya Wamarekani kupitia (Usaid), Wizara ya Afya Ustawi wa
Jamii na MFDI. Alisema kuwa sehemu hii ndiyo inatoa majibu ya msimu wa
kwanza na kuwataka mashabiki watamthilia hii kuangalia TBC kuanza saa
12.30 jioni kupitia TBC.
“Msimu
wa kwanza wa tamthilia ya Siri ya Mtungi uliwavutia watu wengi wa
ukanda wa Afrika Mashariki na kuwaachia maswali kibao na hii imetokana
na tamthilia kubeba vionjo halisi vya maisha katika jamii na hasa kwa
wakazi wa mikoa ya Pwani ya Tanzania,” alisema Kamin.
Alisema
kuwa mapokeo mazuri kutoka kwa watazamaji kuliwapa nafasi ya kuingia
katika vipengele saba vya tuzo za M-Net Africa Magic Viewers Choice
Awards mwaka 2014 ambavyo ni TV Series, Make Up, Wardrobe, Art
Direction, Sound Editor, Acting, and Indigenous Language Series.
“Msimu
wa kwanza ulikuwa hewani katika vipindi vya miaka miwili tangu mwezi
Desemba mwaka jana kupitia vituo vya televisheni vya ITV/EATV na baadaye
kurushwa hewani kupitia DTV, TV1, MNet Africa Magic, Maisha Magic kabla
ya msimu huu kupitia televisheni ya TBC,” alisema.
Kwa
mujibu wa Kamin, mpaka sasa wanajivunia kupata mapokeo mazuri kwenye
mitandao ya kijamii na hasa facebook kwa kupata mashabiki 200,000 na
kwenye YouTube ambapo tumepata watazamaji zaidi ya 500,000 kwani
tamthilia hii imepata umaarufu mkubwa kwa kutazamwa na mashabiki wengi
kuliko vipindi mbali mbali vya televisheni hapa nchini na ukanda wa
Afrika Mashariki.
Alisema
kuwa Siri ya Mtungi ni hadithi ya Kitanzania ambapo wametumia siku 86
kukamilisha kurekodi. Alisema mbali ya kuwashirikisha waigizaji maarufu
kama yvonne Cherie maarufu kwa jina la Monalisa, pia imewashirikisha
warembo maarufu kutoka Miss Tanzania kama Richa Adhia na Jokate Mwegelo.
“Tumetoa ajira kwa waigizaji 60 ambao walipatikana baada ya mchujo wa watu 2,500,” alisema.
Post a Comment