Hali
ya sintofahamu imeibuka katika mtaa wa Azimio, kata ya Kihonda katika
manispaa ya Morogoro, baada ya mwanamke mmoja, Veronica Madebe, kukutwa
akitaka kumtumbukiza mwanaye wa kiume ambaye ni pacha, mwenye umri wa
kati ya miaka mitano hadi saba kwenye kisima cha maji, kutokana na
kinachosadikiwa kuwa ni imani za kishirikina.
Tukio
hilo limejiri katika eneo hilo la Azimio, baada ya mwanamke huyo kukutwa
na mmiliki wa nyumba kilipo kisima hicho, Dani Haji, akijaribu
kumtumbukiza kisimani mmoja wa watoto wake pacha, kwa madai
yaliyoelezwa huenda ni kupungukiwa akili, ama ni imani za kishirikina.
Amedai
kutumwa na wakazi wawili wa eneo hilo kufanya hivyo, na wakati mwingine
kudai alikuwa kwenye kifungo na alipaswa kutoa kafara ya mtoto wake kwa
kumtupa kisimani ili afunguke baada ya kuokoka kiimani, jambo
lililothibitishwa pia na mmoja wa wajumbe wa serikali za mitaa katika
eneo hilo.
Mmoja
wa familia iliyotajwa na mwanamke huyo kufanya kitendo hicho cha
kikatili, kilichozuiwa na wasamaria wema, anakiri kumfahamu mwanamke
huyo lakini bila kuwa na matatizo yeyote, na alishangazwa na hatua hiyo
na alipomuona aliamua kumvaa yeye na mtoto aliyekuwa amembeba, bila
sababu zozote, hadi alipoamuliwa na kundi la wananchi waliojitokeza.
Wananchi
wa eneo hilo walipigasimu polisi kuomba msaada wa dharura na kumpeleka
mama huyo katika ofisi za mtendaji wa kata ya Kihonda, ambako ulinzi
mkali wa polisi uliimarishwa, na baada ya muda mwanamke huyo alitolewa
na kuingizwa kwenye gari ndogo kwa nia ya kupelekwa polisi, lakini
alifanya vurugu hadi polisi walipoingilia kati na kumpakiza kwenye
difenda na kuondoka naye.
Chanzo:EATV.
Post a Comment