HII
kali! Jamaa mmoja ambaye jina lake halikutambulika mara moja, alikutwa
amelazwa chini akiwa amelewa chapachapa, maeneo ya Mtaa wa Kongo,
Kariakoo jijini Dar, huku kawekewa karatasi kifuani na wahuni ikisomeka;
“for sale” (anauzwa).
Kijana akiwa katika hali ya kutojitambua baada ya kupata ulabu wa Kutosha.Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, mwenzake huyo baada ya kuona swaiba wake hajitambui, aliamua kumshusha maeneo hayo na kumlaza chini kisha kumuwekea karatasi kifuani iliyokuwa na maandishi yaliyosomeka; “for sale”.
Chanzo kiliendelea kuweka wazi kuwa mtu
huyo alianza kuwaambia watu waliokuwa wamekusanyika mahali hapo kuwa
kama kuna mtu ana shida na ‘mtoto’ anapatikana kwa bei ya maelewano huku
akiwakataza kumpepea.
Karatasi ya kumnadi kijana huyo ikisomeka 'For Sale' kifuani mwake.Mapaparazi wetu walifika eneo la tukio na kujionea baadhi ya vijana wa mjini wakitaka kumfanyia kitu mbaya lakini kuna mzee mmoja aliwazuia.
Post a Comment