Producer wa hits mbili za Diamond Platnumz ‘Number One’ na
‘Ntampata Wapi’ alionekana kufurahia mafanikio ya Diamond kwenye tuzo za
Channel O, lakini kitu kimoja hakijakaa sawa moyoni mwake.

Sheddy amesema ameshangazwa baada ya kutoona jina lake likiandikwa kwenye video ya ‘Ntampata Wapi’.
“Biashara kweli ni matangazo na nilitakiwa niandikwe kweli kwenye ile
video, lakini sasa kwa sababu imeshapita na vitu vingi vimeshatokea na
ukiangalia kwenye video international wanafanya hivyo ila mpaka sasa
hivi najaribu kujiuliza sijapata jibu kamili kwanini wanafanya hivyo,”
Sheddy ameiambia E-News ya EATV.
“Ukiangalia video za West Africa za akina Davido, Wizkid wengi
producer wa audio wanakuwa hawaandikwi kwenye video. Sasa sijui wanafuta
ule mfumo wa wenzetu, sifahamu.”
Post a Comment