SONY:Tutaonyesha filamu ya Kim Jong-un

Kampuni ya Sony pictures imesema kuwa itaonyesha filamu ya The interview kuhusu mauaji ya Kim jong-un
Kampuni ya Sony Pictures imesema kuwa inatafuta njia mbadala za kuonyesha filamu ya ucheshi 'The Interview' baada ya kusema kuwa haitaonyeshwa kufuatia shambulizi la mtandaoni lililotekelezwa na Korea Kazkazini.
Kampuni hiyo imesema kwamba ilisitisha maonyesho ya filamu hiyo siku ya krisimasi baada ya kumbi za sinema kusema kuwa hazitaionyesha.
Hatua hiyo inajiri baada ya rais Obama kusema kuwa kampuni hiyo ilifanya makosa makubwa kusitisha maonyesho ya filamu hiyo.
Hatuwezi kuwa na jamii ambayo itakuwa na dikteta mahala fulani ambaye atakuwa akijaribu kuamua nini kitakachoonyeshwa na nini hakitaonyeshwa.

 Filamu ya The Interview ambayo imezua mgogoro kati ya serikali ya marekani na ile ya Korea Kazkazini
Obama ameapa kulipiza kisasi shambulizi hilo la mitandai.
Shirika la ujasusi la FBI limesema kuwa Korea kaskazini ndio iliotekeleza shambulizi hilo,madai ambayo Pyongyang inakataa.
Filamu ya 'The Interview' inaonyesha mauaji ya kiongozi wa Korea Kazkazini Kim Jong-un.

Post a Comment

Previous Post Next Post