Tanzania yapunguza malaria kwa 8%

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Seleman Rashid.
Tanzania imefanikiwa kupunguza malaria kutoka asilimia 18.1 hadi kufikia 9.5 (asilimia 8.6) kwa kipindi cha miaka minne.
Akizungumza na NIPASHE, msemaji wa Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja, alisema ugonjwa wa malaria umekuwa ni tatizo kubwa kwa Taifa na kwamba  juhudi za kuutokomeza kabisa zinaendelea kufanyika.

Alieleza njia ambazo wametumia katika kupunguza ugonjwa huo ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kutumia vyandarua vyenye dawa, kunyunyuzia dawa aina ICON kwenye makazi ya watu ili kuua mazalia ya nayosababisha kuzaliana kwa mbu.

Aidha, Mwamaja alisema serikali ya Tanzani kwa kushirikiana na nchi Cuba ina mpango wa kuangamiza mazalia ya mbu hao kwa kutumia njia za kibaiolojia.

Alieleza kuwa kwa mkoa wa Dar es Salaam jumla ya kata 17 kati ya 90 zimeanza utekelezaji wa kuangamiza mazalia hayo.

Alisema mikoa ambayo imenyunyiziwa dawa ni Mwanza, Kagera na Mara huku asilimia 90 ya makazi ya watu ikiwa imeshafikiwa na zoezi hilo katika awamu ya kwanza.

Alisema kwamba awamu yapili inaendelea kwa mikoa ya Shinyanga, Pwani, Lindi, Mtwara na Ruvuma.

 
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

Previous Post Next Post