Wanaume 28 wameshtakiwa kwa kufanya uashertai nchini Misri
Watu
28 wamefikishwa mahakamani mjini Cairo Misri kutokana na mashtaka ya
uasherati katika kile kinachoonekana kama ishara za kampeni dhidi ya
ushoga.
Baadhi ya washtakiwa walikuwa wakilia baada ya kufikishwa mahakamani wakiwa wamefungwa pingu.
Mmoja alilalama kwamba yeye na wafungwa wenzake walipigwa na polisi.
Wanaume hao walikamatwa mapema mwezi huu katika kidimbwi cha kuoga kwa jina hammam mjini Cairo.
Wanahabari wa chombo kimoja cha habari walichukua filamu ya uvamizi huo wa polisi.
Miezi
miwili iliopita,watu wanane walifungwa miaka 3 jela baada ya kunaswa
katika kanda ya video ambayo wakuu wa mashtaka wanasema ilionyesha
wakifanya harusi ya watu wa jinsia moja mjini Cairo.CHANZO BBC SWAHILI
Post a Comment