Wanawake
saba wameuawa katika mashambulizi ya 'kinyama' nchini Somalia baada ya
wanamgambo wa al-Shabaab kumchinja mke wa mwanajeshi.
Hatua hiyo ilikuja ili kulipiza kisasi kwa wanawake walio na uhusiano wa karibu na wapiganaji hao wenye itikadi kali.
Kwa mujibu wa DW, mmoja
kati ya mateka hao alikuwa ni mke wa mwanajeshi na mwingine mpishi wa
majeshi ya Serikali na kuwakata vichwa wote.
Katika kulipiza kisasi
mwanajeshi aliyefiwa pamoja na wenzake waliwakamata wanawake kumi
waliosema ni wake za wapiganaji wa al-Shabaab na kuwaua watano kabla ya
wazee kuingilia kati na kuwaokoa wengine.
- Majira
Post a Comment