Inaendelea kutoka wiki iliyopita. Albert Pike alifanya kazi zake
kwa ukaribu na Giusseppe Mazzini wa Italia (1805-1872) ambaye alikuwa
ni mwashi huru mwenye digrii 33, ambaye alikuwa ni mkuu wa Illuminati
mnamo mwaka 1834, na ndiye mwanzilishi wa kundi la Mafia mnamo mwaka
1860.
Wengine aliofanya nao kazi kwa ukaribu ni Adriano
Lemmi (1822-1896) na baadhi ya viongozi mashuhuri wa ulimwengu kama vile
Lenin, Trosky na baadaye Stalin, lengo likiwa ni kuziangusha tawala
mbalimbali za kifalme za Ulaya na kuanzisha tawala za kimapinduzi yakiwa
ni maandalizi ya kuanzisha utawala mmoja tu ulimwenguni. Huu ulikuwa ni
mwendelezo wa falsafa ya illuminati ambayo ilianzishwa na Adam
Weishaupt.
Kati ya mwaka 1859 hadi 1871 aliandaa mpango
mkakati wa kuanzisha vita kuu tatu za dunia na mapinduzi matatu makubwa
akitabiri kuwa matukio yote hayo yangetokea katika karne ya 20.
Ili yaliyotabiriwa yatokee kama ilivyopangwa, Pike
aliamini kuwa falsafa za Ukomunisti, Ufashisti na Uzayuni, ambazo ni
matokeo ya kazi za waashi huru, zingetumika kuchochea vita na mapinduzi
duniani.
Ikumbukwe kuwa mnamo mwaka 1829 katika mkutano wao
wa New York, waashi huru walitangaza kuwaunganisha watu wote wasioamini
uwepo wa Mungu katika mwavuli mmoja wa Ukomunisti. Karl Marx na
Friedrich Engels walifadhiliwa fedha ili waandike vitabu vitakavyoweka
msingi wa itikadi ya Ukomunisti.
Wakati Marx na Engels wakiandika kuhusu nadharia
ya ukomunisti, waashi huru walimwajiri mwanafalsafa Friedrich Wilhelm
Nietzsche kuandika nadharia inayopingana na ukomunisti ambayo inaonyesha
ubora wa watu wa asili ya Aryan.
Lengo la waashi huru kuwapa kazi waandishi hawa
kuandika nadharia mbili kinzani ni kuleta mgogoro miongoni mwa wafuasi
wa nadharia hizo, hivyo kuleta vita vitakavyopelekea kuanguka kwa
nadharia mojawapo. Pia hiki ndicho kilichotokea kwenye vita kuu ya pili
ya dunia.
Pike alitabiri vita kuu ya kwanza ya dunia ambayo
alisema ilikuwa ni muhimu ili kuuangusha ufalme uliodumu kwa miaka 3000
wa ukoo wa Romanov kule Urusi ili kuifanya Urusi kuwa ni ngome ya
Ukomunisti.
Vita hivi vilitokea mwaka 1914-1918 vikifuatiwa na mapinduzi ya Kikomunisti kule Urusi mnamo Oktoba 1918.
Alitabiri Vita Kuu ya Pili ya Dunia, ambayo
alisema lengo lake ilikuwa ni kuongeza nguvu ya Uzayuni wa kisiasa na
kuanzisha Dola ya Israeli kule Palestina na kuufanya Ukomunisti uwe na
nguvu zaidi ya Ukristo. Vita hivi vimetokea kama lilivyotabiriwa.
Vita kuu ya tatu ya dunia ilitabiriwa kuwa
ingetokea kutokana na sintofahamu zilizopo kati ya uzayuni wa kisiasa na
ulimwengu wa Kiislamu lengo likiwa upande mmoja kuuharibu mwingine.
Vita hivi bado havijatokea japo ishara za kuzuka
kwake zipo bayana ukiangalia yanayotokea sehemu mbalimbali za dunia
hususan kule Mashariki ya Kati na namna mataifa makubwa yanavyofanya
dhuluma mbalimbali dhidi ya mataifa madogo ikiwemo unyonyaji wa
rasilimali zao,
- Mwananchi
- Mwananchi

Post a Comment