Mkurungezi
wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Asha Baraka amemuonya msanii
anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’
kutojaribu kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya na kusema
akijaribu atapotea.
Mkurungezi wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Asha Baraka.
Akizungumza
na Ijumaa hivi karubini, Asha Baraka ‘Iron Lady’ alisema Diamond
anaweza kufanya vizuri kwa miaka mingi inayokuja lakini akijaribu
kutumia dawa hizo ataishia pabaya.
“Tumeona
wasanii wengi wa Tanzania ambao awali walikuwa wanafanya vizuri lakini
baada ya kujaa sifa na kukutana na marafiki wengi pamoja na makundi
wakazama kwenye dawa za kulevya na sasa wanatapatapa na kubaki kulaumu
wakati wenyewe wamejiharibia,” alisema Iron Lady.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Wasani
ambao awali walikuwa wakifanya vizuri kimuziki lakini baadaye
‘wakadrop’ baada ya kujiingiza kwenye matumizi ya unga ni pamoja na Chid
Benzi, Ray C, Q Chiller, Lord Eyez, Msafiri Diof na wengine ambao sasa
wameshafariki.
Post a Comment