Mfanyabiashara wa mbao Manispaa ya Songea, Emmanuel Moshi (40), mkazi wa Marangu, mkoani Kilimanjaro amemuua mfanyabiashara mwenzake aliyetambuliwa kwa jina la Didas Alphonce (64), mkazi wa Kilema Kilimanjaro kwa kumpasua kichwa kwa shoka, kisha yeye mwenyewe kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani katika stoo ya nyumba waliyokuwa wakiishi.
Inadaiwa kuwa Moshi alichukua uamuzi huo baada ya Alphonce kumdhulumu zaidi ya Sh87.4 milioni.
Wakizungumza
na Mwandishi jana, watu wa karibu na wafanyabiashara hao ambao
hawakupenda majina yao kuandikwa, walidai kuwa
wafanyabiashara hao walikuwa wakiishi nyumba ya ndugu yake, Didas na
kufanya biashara za kuuza mbao pamoja.
Walidai kuwa,
Desemba 30 mwaka jana, wafanyabiashara hao walikuwa wakinywa pombe
kwenye Bwalo la Magereza na Moshi alikuwa akilalamika kudhulumiwa na
Didas.
Mashuhuda hao waliongeza kuwa tangu siku hiyo, wafanyabiashara hao hawakuonekana tena hadi jana.
Ilidaiwa kuwa, mwenye nyumba huyo alitumia funguo zake za akiba
kufungua nyumba hiyo na kukuta mwili wa mjomba wake ukiwa umepigwa na
shoka na tayari umeanza kuharibika.
Mtu mmoja ambaye
jina lake tunalihifadhi alitoa taarifa kituo cha polisi na walipofika
waliubaini pia mwili wa Moshi aliyejinyonga.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela alithibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kudai uchunguzi wa awali unaonyesha wafanyabiashara hao walikuwa
wanadaiana pesa.
Alisema Mosha ameacha ujumbe mrefu wa karatasi nne aliouandika kuhusiana na mauaji hayo.
Ujumbe
huo: “Kataeni wadhulumaji kati ya matajiri na maskini, nimeondoa dhambi
kubwa ya dhuluma iliyokuwa ikinitesa ulimwenguni, wadhulumaji
wasifumbiwe macho jamii iniunge mkono kuondoa watu hawa.
“Dhuluma aliyonifanyia mtu huyu imekatisha maisha yangu.”
“Dhuluma aliyonifanyia mtu huyu imekatisha maisha yangu.”
Post a Comment