Maandamano nchini Pakistan kuonyesha kero la waumini wa kiisilamu kuhusu Charlie Hebdo.
Polisi
nchini Pakistan wamekabiliana na waandamanaji, walioghadhabishwa na
uamuzi wa jarida na Ufaransa la Charlie Hebdo wa kuchapisha vibonzo vya
mtu wanayedai ni Mtume Mohammad.
Baada ya
maombi ya ijumaa, maafisa wa ulinzi walitumia magari yenye majai
kuwamwagia maji waandamanaji katika juhudi za kuwatwanya.
Walikuwa wamekusanyika nje ya ubalozi wa Ufaransa mjini Karachi.
Baadhi ya waandamanaji inaarifiwa walikuwa wamebeba bunduki. Watu watatu walijeruhiwa katika maandamano yenyewe.
Mwandishi
wa BBC mjini Islamabad amesema idadi ya waandamanaji hao, kwa mujibu wa
idadi ya wasisilamu nchini Pakistan, ilikuwa ndogo.
Maandamano
kama hayo yameitishwa katika nchi zingine zilizo na idadi kubwa ya
waumini wa Kiislamu kama vile Uturuki, Ufilipino,Kuwait, Mauritania na
Sudan.
BBC.
Post a Comment