HATIMAYE
Miss Ruvuma 2008 ambaye pia ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva na
filamu Bongo, Isabela Mpanda ‘Bela’, ameweka wazi kuwa hataki tena ndoa.
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na filamu Bongo, Isabela Mpanda ‘Bela’.
Akizungumza na Uwazi, mwandishi wetu Bela alisema amefikia hatua hiyo
baada ya kukaa kwa muda mrefu akisubiri ndoa bila mafanikio na
maendeleo yoyote na kuishia kudharaulika katika jamii.
“Sitaki tena ndoa kwa sasa hivi ila ninachohitaji ni kupumzika, hata
akitokea mtu siko tayari kwa sasa. Nilishasubiri sana ndoa mpaka hamu
imeniisha,” alisema Bela

Post a Comment