Wanajeshi wa serikali waliokuwa wakipiga doria katika mji wa
Baga kabla ya Boko haram kuuteka pamoja na kambi ya kijeshi
Maafisa nchini Nigeria wanasema kuwa kundi la Boko Haram
limeuteka mji na kambi moja ya kijeshi inayotumiwa na wanajeshi wa kimataifa
wanaojaribu kukabiliana na wapiganaji hao.
Seneta wa Borno Kazkazini Maina Ma'aji Lawan,eneo la mji wa
Baga amesema kuwa wanajeshi waliitoroka kambi yao baada ya kushambuliwa na Boko
Haram jumamosi asubuhi.
Wakaazi wa Baga,ambao walitoroka kupitia maboti hadi taifa
jirani la Chad,amesema kuwa raia wengi wameuawa na mji huo kuchomwa.
Post a Comment