Kamanda wa kundi la waasi la LRA
nchini Uganda ambaye alijisalimisha katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati,
Dominic Ongwen atakabidhiwa kwa mahakama ya kimataifa ya ICC, yasema
serikali ya Uganda.
Kamanda huyo ni miongoni mwa watu wa kundi la
LRA wanaosakwa na viongozi wa mashitaka katika mahakama ya kimataifa ya
ICC kwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu.
Ongwen alikabidhiwa wanajeshi wa Marekani wiki jana na bado anazuiliwa na wanajeshi hao.
Marekani
ilikuwa imeahidi kutoa kitita cha dola miliono 5 kama zawadi kwa
atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwa kamanda huyo,
kuhamishwa kwake na hatimaye kufunguliwa mashitaka.
Maafisa wakuu nchini Uganda wanasema kwamba Ongwen atapelekwa nchini Uganda katika siku chache zijazo.
Anajaulikana
kwa jina "White Ant", jina lake la msituni na yeye ndiye naibu kamanda
wa kundi la LRA Joseph Kony ambaye pia anasakwa na mahakama ya kimataifa
ya ICC.
Kundi la LRA liliwateka nyara maelfu ya watoto na kuwalazimisha kupigana huku wasichana wakifanywa watumwa wa ngono.

Post a Comment