Makali ya mwanamitindo na mlimbwende Kim Kardashian yamekuwa gumzo kubwa duniani kote
Fumbo
la siku zote kwamba wanawake ni wanene kuliko wanaume limepata
ufumbuzi...ni wanene kwa wanahitaji mwili wenye umbo zuri na makalio
makubwa ili kupata watoto waliojaaliwa werevu.
Taarifa hii ni kwa
mujibu wa wanaakademia ambao wanasema kuwa wanawake wenye makalio na
mapaja makubwa na umbo zuri kutokana na mafuta mfano kama
Kim Kardashian hupata watoto werevu.
Nini hasa kinawafanya
watoto wao kuwa werevu basi? Mafuta yanayopatikana katika sehemu za
mwili wa mwanamke huwa na manufaa makubwa sana kwa watoto hasa
wanapokuwa wananyonya, mafuta haya hupitia kwenye maziwa ya mama hadi
kwa mwili wa mtoto.
Profesa Will Lassek wa chuo kikuu cha
Pittsburgh University, Pennsylvania, aliyeongoza utafiti huo, anasema
mafuta yanayopatikana katika sehemu hizo za mwili, husaidia sana katika
kukuza ubongo wa matoto mchanga.
Ubongo wa binadamu
'Unahitaji mafuta mengi ya
mwilini ili kuwa na mfumo mzuri wa neva na mafuta katika sehemu hizi za
mwili yaani mapaja na makalio, huwa yina madini yajulikanayo kama DHA
(docosahexaenoic acid), ambayo ni muhimu sana katika kutengeza ubongo wa
binadamu.
Inaonekana kama wanawake wameweza kujua mbinu za kuhifadhi mafuta katika sehemu hizo za mwili hadi wanapopata mtoto.
Kwa
mda mrefu haijajulikana kwa nini wanawake wanakuwa wanene
sana.......mafuta ya mwili wao yakiwa ni asilimia 30 ya uzani wa mwili.
Professa
Lassek anasema kwamba mafuta hayo ni kiwango sawa na yale
yanayopatikana katika wanyama kama Dubu au Nyangumi wanapojiandaa kuzaa.
Wanasayansi
wanasema mafuta yanayopatikana katika mapaja na makalio ya wanawake
ndio yanayotumika kutengeza ubongo wa watoto wachanga.
Mafuta
mengi katika mwili wa mwanamke huisha mwilini pindi mama anapomnyonyesha
mtoto wake, kulingana na Profesa Lassek, aliyechapisha utafiti wake
katika kitabu chake kipya chenye kichwa ''Kwa nini wanawake wanahitaji
mafuta mwilini. ''
Wanawake wanaonyonyesha hupoteza kilo nusu ya mafuta mwilini kila mwezi.


Post a Comment