Hali tete bomba la gesi Mtwara

Kigogo adaiwa kuzuia mshahara wake, kuongeza mkataba
* Uongozi wafunguka
Mwandishi Wetu
MMOJA wa viongozi wa juu wa  Klabu ya Simba anadaiwa kuzuia mshahara wa mlinzi wa timu hiyo, Mganda Joseph Owino wakati wachezaji wenzake wote wakiwa wamelipwa.
Habari za uhakika ilizonazo Jambo Leo, hadi juzi mchezaji huyo alikuwa hajapata mshahara wake mwezi uliopita, ambapo ameambiwa atapewa Alhamisi ijayo ikiwa haijulikani ni kwa sababu gani.
Chanzo cha uhakika kililiambia gazeti hili kuwa Owino ambaye ni majeruhi, anaonekana kama hana mchango wowote katika klabu hiyo kutokana na kuwa kwake nje ya kambi huku kiongozi huyo akidaiwa kumpa maneno makali ya kumtisha.
Moja ya vitisho vinavyodaiwa kutoka kwa kiongozi huyo aliyechaguliwa katika mkutano mkuu uliopita ni kutochezea tena Simba, yeye akiwa kama kiongozi ndani ya klabu hiyo.
Mtoa habari huyo alisema hivi karibuni viongozi wengine walianza mazungumzo na mchezaji huyo ambaye ni nahodha wa timu hiyo kwa ajili ya kusaini mkataba mwingine, lakini ameonekana kutokuwa tayari kutokana na chuki alizokuwa nazo kiongozi huyo.
Alisema hivi karibuni Owino alikutana na viongozi wakuu wa klabu hiyo akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya usajili, Zakaria Hans Pope, ambao walizungumzia mkataba mpya wa kuitumikia klabu hiyo, lakini  imekuwa ngumu kwa sababu ya kuwepo bifu (kutoelewana) kati yake na kiongozi huyo ambaye hamtaki huku ikielezwa kuwa kiongozi mwingine katika benchi la ufundi la timu hiyo anaonekana kuunga mkono .
Alisema hata kutoonekana uwanjani kwa nyota huyo kumechangiwa na kiongozi huyo, ambaye aliwahi kumshinikiza  aliyekuwa kocha wa timu hiyo kabla ya kuondolewa, Patrick Phiri asimpange kwenye kikosi cha kwanza.
“Tatizo kwenye benchi kuna kiongozi anayemuunga mkono kiongozi huyo wa kuchaguliwa kumwekea ngumu, Owino asicheze, kitu ambacho hata yeye amekiona ndiyo maana anataka kutoka akaangalie mambo yake mengine,”kilisema chanzo hicho.
Owino aliponea chupuchupu kuachwa kwenye usajili wa dirisha dogo kutokana na mchezaji aliyetakiwa kuchukua nafasi yake (David Owino ‘Calabar’) kushindwa kusaini kwa wakati ikidaiwa kuwa hakuwa tayari kujiunga na Simba.
Hata hivyo imesemekana usajili huo ulikuwa na lengo la kumkomoa mchezaji huyo, ambaye kwa sasa anatakiwa na moja ya timu  iliyopo Dubai Falme za Kiarabu.
Kiliongeza chanzo hicho kuwa wakati wachezaji wengine wa Simba wanapewa mshahara juzi, Owino aliambiwa atapewa wiki ijayo kwa sababu  fedha zilikuwa zimeisha.
“Ni kweli wenzake wote wamepewa lakini yeye akaambiwa mpaka wiki ijayo, eti fedha ziliisha, tatizo kuna kiongozi hapa  anatofautiana naye, hatujui anatatizo naye gani, alisema mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo.
Jambo Leo lilipowasiliana na Katibu Mkuu wa Simba, Steven Ali kujua kama ni kweli kuhusu Owino kutopata mshahara, alikiri kuwa anadai wa mwezi mmoja.
Ali alisema anachojua ni kwamba Owino alikosa mshahara kwa kuwa hakuwepo kambini , lakini mambo mengine hayajui.
“Ninachojua Owino alikosa mshahara kwa sababu ya kutokuwepo kambini na sio vinginevyo, lakini hayo mengine mi siyajui,” alisema Owino

Post a Comment

Previous Post Next Post