Askari
wanaolinda pwani ya Italia wanajaribu kuwasaidia watu waliokwama ndani
ya meli moja ya kibiashara, iliyotelekezwa katika pwani ya kusini
mashariki mwa nchi hiyo.
Meli hiyo ina zaidi ya wahamiaji haramu wapatao mia nne. Hakuna mhudumu yeyote au nahodha kwenye meli hiyo.
Hali
mbaya ya hewa inaripotiwa kukwamisha shughuli za uokoaji, ambapo watu
hao wanajaribu kuhamishiwa ndani ya meli ya Sierra Leone, inayobeba
mifugo.
Post a Comment