Kiongozi wa upinzani apinga kufuatiliwa

Kiongozi wa upinzani Urusi, amekatilia mbali kifaa cha elektroniki kufuatilia nyendo zake ikiwa ni kupinga adhabu aliyopewa.
Alexei Navalny alituma picha ya kifaa hichoalichokuwa amevalishwa katika blog yake, akisema anakataa "kuzuiliwa kwake kusikofuata sheria" na kwamba kuhukumiwa kwake kwa ufujaji wa fedha za umma kulifanyika kinyume cha sheria.
Navalny alipewa kifungo cha nje kwa kuzilaghai kampuni mbili mwezi Desemba.
Amesema kesi dhidi yake zinachochewa na upinzani alionao dhidi ya Rais Vladimir Putin.
Navalny amekuwa akizuiliwa nyumbani kwake tangu mwezi Februari 2014.
Katika taarifa aliyoituma kwenye blog yake anasema: "sina mipango ya kusafiri kokote kule, ninachohitaji kuhusiana na kutembea ni kuweza kutembea kutoka nyumbani hadi ofisi na kurudi, na kutumia muda wangu na familia yangu."
Ameandika kuwa "ni mtu pekee katika historia ya mahakama ya Urusi" kubakia katika kifungo cha nyumbani baada ya kuhukumiwa

Post a Comment

Previous Post Next Post