Chama cha wafugaji nchini (CCWT) kimeitaka serikali kutoa kauli juu
ya mauaji ya ng’ombe zaidi ya 5480 yaliyofanywa na askari wa wanyamapori
kutoka hifadhi ya taifa ya mbuga ya katavi kwa kipindi cha miaka miwili
kufuatia vitendo hivyo kuendelea kila kukicha ambapo hivi karibuni
ng’ombe 52 wamepigwa risasi na askari hao huku kukiwa hakuna hatua
zozote zinazochukuliwa.
Kauli hiyo inatolewa na katibu wa chama cha wafugaji tanzania
(CCWT) George Kifuko ambapo amesem,a chama hicho kinalaani mauaji ya
ng’ombe ambayo yamekuwa yakifanywa na askariw a wanyamapori kila kukicha
kwa kisingizio cha ng’ombe kuingika katika hifadhi ambapo kwa kipindi
cha mwaka 2012 mpaka 2014 katika mkoa wa katavi pekee jumla ya ngombe
5480 wameuwawa kwa kupigwa risasi na askari wa wanyamapori wa mbuga ya
katavi.
Katibu huyo pia akaonya baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa
wakiwatumia viongozi waliosimamishwa katika chama hicho kujenga migogoro
kwa maslahi yao binafsi kwa kuwagawa wafugaji kikabila na kikanda hali
ambayo inaweza kuzua migogoro mkubwa katika jamii hiyo.
- ITV
Post a Comment