
Meli
kubwa zaidi duniani imetia nanga nchini Uingereza kwa mara ya kwanza
wakati huu ikiendelea na safari yake duniani, je Meli hii ina nguvu
kiasi gani na ukubwa gani?
Meli iitwayo the Globe ina urefu wa
mita 400 ikifananishwa na ukubwa wa mabwawa manane yanayotumika katika
michuano ya Olimpiki ina upana wa mita 56.8 na upana wa mita 73 kwenda
juu, ina uwezo wa kubeba mzigo wa tani 186,000.Safari ya Meli hiyo ilianzia mjini Qingdao nchini China tarehe 3 mwezi Desemba mwaka jana na inatarajiwa kumaliza ziara yake tarehe 25 Februari.


Post a Comment