Mbunge wa jimbo la Kigoma kusini David Kafulila amesema wananchi
wanataka kuona serikali inawafukuza kazi na kuwafikisha mahakamani
vigogo wote waliohusika katika sakata la wizi wa fedha za Tegeta Escrow
kwani waliofikishwa mahakamani mpaka sasa ni viongozi wadogo huku
vigogo wakubwa wa serikali waliohusika na wizi wa fedha wakipewa
likizo ya kutumia fedha hizo.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya tungi manispaa
ya Morogoro mbunge wa jimbo la Kigoma kusini kwa tiketi ya NCCR mageuzi
Davidi Kafurila amesema wananchi wanataka kuona vigogo waliohusika
katika sakata la wizi wa fedha za Escrow kufukuzwa kazi, kurejesha fedha
hizo na wapelekwe mahakamani na si kuwapeleka watu wadogo huku vigogo
wakipewa likizo ya kutumia fedha hizo.
Naye naibu katibu mkuu wa Bawacha taifa kunti Yusufu amewataka
wananchi wa Morogoro kuchukua hatua madhubuti juu ya ustawi wa taifa kwa
kujitokeza kujiaandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura ili
kupata fursa ya kuchagua viongozi watakaoweka mbele maslahi ya wananchi
na kuwakumbusha wananchi wasidanganyike kupigia kura katiba
inayopendekezwa kwani katika hiyo imeweka mbele mashlahi ya vigogo na
kuacha kando matatizo ya wananchi.
Post a Comment