Mtoto mwenye matatizo ya tumbo, Suleiman Abdallah.
Makala: Shani RamadhaniWANAMKE mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Veronica Laurent, mkazi wa Magomeni Mwembechai, jijini Dar, amejikuta kwenye wakati mgumu kwa kutelekezwa na mzazi mwenzie baada ya kujifungua mtoto akiwa na matatizo ya utumbo.
CHOO CHATOKEA MDOMONI
Akizungumza na mwandishi wetu Veronica alisema mwanaye Suleiman Abdallah (4), alipozaliwa tu, choo chake hakikutoka kwa njia ya kawaida bali kilitokea mdomoni huku manesi wakisema ana utumbo mkubwa na moja kwa moja alichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na hali yake kuwa mbaya.
![](http://api.ning.com:80/files/kBk*s0lw*Nm3KmUVGK4TlTi3HVtuXtWk38rQ8gIKH1Emhj84U8Ti1A486rkmjc2Gm2j651ElqDk594vosJSIiCBitT-m64et/IMG_20150102_165647.jpg)
Sehemu ya tumbo la mtoto Suleiman Abdallah iliyofanyiwa upasuaji.
AWEKEWA UTUMBO WA PLASTIKI“Tulipofika pale Muhimbili mwanangu aliwekewa mashine ya kupumulia na baada ya kumchukua vipimo waligundua kuwa utumbo mkubwa wa choo umejifunga wakasema itabidi alazwe kwa ajili ya upasuaji ambapo alipasuliwa na kuwekewa utumbo wa plastiki ambao anaishi nao mpaka leo.
“Sasa tukaandikiwa tuwe tunahudhuria kliniki kila mwezi kutokana na tarehe husika lakini mwezi uliopita mtoto alianza kulalamika kuwa anasikia maumivu makali ya tumbo na hapati choo kabisa na hata akipata ni kidogo sana.
![](http://api.ning.com:80/files/kBk*s0lw*Nn5Wg4l-QaaRP6M2o10NbkhpXVA1uNe*4VVlnGfRjDuAGpBzkJVfK7Uw3W*rgJiuR*axGStmxRblU*zIL1Ck-qI/IMG_20150102_170415.jpg)
Kovu la upasuaji tumboni mwa mtoto Suleiman Abdallah.
“Tulienda hospitali tukapewa dawa za kutuliza maumivu tu na madaktari
walishasema kama mtoto ana maumivu ya tumbo tumpeleke kwenye hospitali
ya karibu, Muhimbili ni kwa ajili ya kliniki yake tu,” alisema mama huyo
huku akitokwa machozi.BABA AMTELEKEZA
Mama huyo anaelezea kuwa yeye ndiye mlezi wa mtoto huyo baada ya kutelekezwa na mzazi mwenzie ambaye alidai hajali kumhudumia.
“Baba wa mtoto alipoona mwanaye ana matatizo haya alisema hanihitaji mimi na mtoto niende nikatafute mtu wa kunisaidia na yeye atatafuta mwanamke mwingine wa kuzaa naye pia nilishawahi kupigwa na shangazi yake kwa madai kuwa namsumbua mwanaye.
![](http://api.ning.com:80/files/kBk*s0lw*Nmz73wOk9QcqyvBJZJfsekq2yNa*chFx2jgtWkAwy2szvWnRr-pwisskzYcHWOtwr6PdAjDJw8uiQBphV0wcLTv/IMG_20150102_165752.jpg?width=650)
Veronica Laurent ambaye ni mama mzazi wa mtoto Suleiman Abdallah.
APASULIWA MARA NNE“Nimekuwa nikihangaika mwenyewe kwa miaka yote tangu alipozaliwa na tayari ameshapasuliwa mara nne tangu azaliwe lakini bado tatizo linaendelea kumtesa mtoto.
“Kwa sasa naomba serikali inisaidie kama inawezekana naomba mwanangu achunguzwe tena kwa sababu sasa hivi analalamika sana na hata tumbo lake linajaa,” alisema na kuongeza kuwa ili apasuliwe tena zinahitajika fedha shilingi 1,000,000 ambazo hana hata senti tano.
Ili kuweza kufanikisha upasuaji huo wewe uliyesoma habari hii unaombwa kumsaidia mama huyu kwa kiasi chochote ulichonacho na Mungu atakupa baraka zake.
Aliyeguswa na kuhuzunishwa na mateso ya mtoto Suleiman anaweza kuchangia kupitia namba ya simu 0712 004 677 na 0767 026 551.
Post a Comment