Mwakyembe: Mipasuko na makundi ndani ya CCM yatadhoofisha uchaguzi

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe amesema sababu zinazofanya CCM   kupoteza kura  katika uchaguzi mkuu wa urais na wabunge mwaka huu ni pamoja na kuwa na mipasuko ama makundi ndani ya chama .
 Mwakyembe aliyasema hayo juzi wakati akizungumza  na wanahabari pamoja na kutembelea taasisi zilizo chini ya wazira yake,  ikiwamo  uwanja wa ndege wa Nduliwa mjini Iringa.

Pamoja na kutembelea uwanja huo  na baadae kuzungumza na wadau wa usafiri wa mkoani hapa, aliwataka viongozi wa mamlaka ya viwanja vya ndege mkoani Iringa  kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa kushughulikia tatizo la wavamizi wa eneo la uwanja.

Alisema kuwa uwanja wa ndege wa Iringa ni miongoni mwa viwanja 11 ambavyo vipo katika mpango wa kufanyiwa marekebisho makubwa katika awamu hii ya mpango wa ujenzi

 “Serikali sasa hivi ina miradi mingi  inajenga miundombinu ya viwanja vya  ndege ili watu wengi waweze kunufaika na huduma ya usafiri wa anga ,tumemaliza uwanja wa Mpanda na Mafia tunajenga wa  Kigoma  na umefikia kwenye jengo la abiria.

“Kwa kuwa ni kiwanja cha mpakani tumeamua kurefusha uwanja kufikia kilometa  tatu  ili kiwe na uwezo wa kubeba abiria 150”alisema  Mwakyembe na kuongeza:

“Tunaendelea na upanuzi wa uwanja wa Ndege wa Mwanza ambao utakuwa mkubwa kuliko vingine Afrika Mashariki tunajiandaa kukarabati uwanja wa Kilimanjaro na Songwe mkoani Mbeya”

Alisema Uwanja wa  Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam nao unaendelea.
 
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

Previous Post Next Post