INASIKITISHA!
Mtoto Seif Sudi Seif, 15, (pichani), wa Shule ya Msingi Hedenzeri,
Tanga analia kwa uchungu akitaka kusaidiwa ili aweze kutimiza ndoto zake
kutokana na tatizo lake la kushindwa kutembea kutokana na kuumwa
mgongo.
Mtoto Seif Sudi Seif akishindwa kutembea kutokana na tatizo la mgongo.
Mama wa mtoto huyo, Fatuma Hemed aliliambia gazeti hili akiwa
nyumbani kwa shemeji yake maeneo ya Uwanja wa Ndege jijini Dar,
alikofikia akitokea Tanga, kuwa tatizo la mwanaye lilianza miaka minne
iliyopita na sasa anashindwa kutembea.
Akifafanua zaidi alikuwa na haya ya kusema: “Kabla ya mwanangu
hajakumbwa na tatizo hili alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kuanguka
akidai kuona kizunguzungu hadi kushindwa kabisa kutembea na sasa
hushinda amelala, anashindwa hata kuinuka.
“Ni tatizo zito na kwa upande wa masomo anajitahidi sana katika
mitihani yake shuleni japokuwa anapata shida kubwa ya kukokota baiskeli
ya kusukuma kutokana na mgongo wake kutokuwa imara kusimama,” alisema
mama huyo.
Mtoto Seif Sudi akiwa na mama yake.
Naye mtoto Seif alisema kuwa anatamani sana kurudia katika hali yake
ya zamani na angependa kutimiza ndoto zake za kusoma hadi chuo
kikuu.“Lakini ndoto hizo nitashindwa kutimiza kutokana na kuumwa na sasa
nashinda kitandani nimelala bila kuinuka wala kutembea.
“Mama amenipeleka hospitali mbalimbali kama vile Mkoa wa Tanga,
Hospitali ya Mombo pamoja na Dar, Hospitali ya CCBRT, Tumbi ya Kibaha
lakini imeshindikana kwa kuwa hata hivyo, uwezo hana.
‘’Nawaombeni Watanzania mnisaidie niweze kutimiza ndoto zangu kwani nimehangaika sana, mama yangu amehangaika,’’ alisema Seif.
‘’Nawaombeni Watanzania mnisaidie niweze kutimiza ndoto zangu kwani nimehangaika sana, mama yangu amehangaika,’’ alisema Seif.
Mama wa mtoto huyo alisema ameambiwa na madaktari kuwa tatizo la
mwanaye ni ‘mgongo kusogea’ na anaweza kutibiwa nchini India.Yeyote
atakayeguswa na tatizo hilo awasiliane na mama wa mtoto kwa namba 0653
542 128 au 0715 125 703 Fatuma Hemed.
Post a Comment